Numbers 31:52 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumla ya dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu ilikuwa karibu kilo 200.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Musa na kuhani Eleazari walimletea Mwenyezi Mungu kama zawadi ilikuwa shekeli elfu kumi na sita, mia saba na hamsini (16,750).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa Bwana, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na sita elfu na mia saba na hamsini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumla ya dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu ilikuwa karibu kilo 200.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimletea BWANA kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Musa na kuhani Eleazari walimletea bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa BWANA, ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, ilikuwa shekeli elfu kumi na sita, mia saba na hamsini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumla ya dhahabu yote waliyomtolea Mwenyezi-Mungu ilikuwa karibu kilo 200.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo dhahabu zote, walizomtolea Bwana kuwa vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa zilikuwa frasila kumi na saba, ndizo zilizotoka kwa wakuu wa maelfu na kwa wakuu wa mamia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa BWANA, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na sita elfu na mia saba na hamsini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jumla ya zahabu yote waliyomutolea Yawe ilikuwa karibu kilo mia mbili.