Numbers 31:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli waliteka nyara: Ng'ombe, kondoo na mali yao yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli waliwateka wanawake wa Midiani pamoja na watoto wao, na wakachukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali yao kama nyara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli waliteka nyara: ng'ombe, kondoo na mali yao yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng'ombe, kondoo na mali zao kama nyara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali zao kama nyara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe wao wote, na kondoo wao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli waliteka nyara: Ng'ombe, kondoo na mali yao yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wana wa Isiraeli wakawateka wanawake wa Midiani na watoto wao, nao ng'ombe wao wote na mbuzi na kondoo wao wote na mali zao zote pia wakazichukua kuwa nyara zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng’ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wakawapeleka kuwa wafungwa wanawake wa Midiani na watoto wao. Wakanyanganya: ngombe, kondoo na mali yao yote.