Numbers 32:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hatutamiliki mali yoyote miongoni mwao ngambo ya mto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ngambo hii, mashariki ya mto Yordani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ng’ambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki mwa Yordani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani kwa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hatutamiliki mali yoyote miongoni mwao ng'ambo ya mto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ng'ambo hii, mashariki ya mto Yordani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hatutapokea urithi wo wote pamoja nao ng'ambo ya pili ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ng’ambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa mashariki mwa Yordani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hatutamiliki mali yoyote miongoni mwao ngambo ya mto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ngambo hii, mashariki ya mto Yordani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sisi hatutapata mafungu pamoja nao ng'ambo ya huko ya Yordani pande hizo za huko, kwani mafungu yetu sisi yametuangukia ng'ambo ya huku ya Yordani upande wa maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng’ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani kwa mashariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hatutarizi mali yoyote kati yao ngambo ya muto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ngambo hii, upande wa mashariki wa muto Yordani.