Numbers 32:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ikiwa watu wa Gadi na wa Reubeni watavuka mto Yordani pamoja nanyi wakiwa na silaha zao chini ya uongozi wa Mwenyezi-Mungu, mkashinda na kuichukua nchi hiyo, basi mtawapa nchi ya Gileadi iwe mali yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za Mwenyezi Mungu, basi mtakapoishinda nchi iliyo mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akawaambia, Kwamba wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu aliyevaa silaha kwa vita, mbele za Bwana, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ikiwa watu wa Gadi na wa Reubeni watavuka mto Yordani pamoja nanyi wakiwa na silaha zao chini ya uongozi wa Mwenyezi-Mungu, mkashinda na kuichukua nchi hiyo, basi mtawapa nchi ya Gileadi iwe mali yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za BWANA, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za bwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akawaambia, Ikiwa wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu akiwa amevaa silaha kwa vita, mbele za BWANA, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ikiwa watu wa Gadi na wa Reubeni watavuka mto Yordani pamoja nanyi wakiwa na silaha zao chini ya uongozi wa Mwenyezi-Mungu, mkashinda na kuichukua nchi hiyo, basi mtawapa nchi ya Gileadi iwe mali yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
yeye Mose akiwaambia: Wana wa Gadi na wana wa Rubeni, ni kwamba: wote wa kwao wanaoweza kushika mata ya vita wakiuvuka Yordani pamoja nanyi machoni pa Bwana, basi, nchi itakapokuwa imetiishwa mbele yenu, sharti mwape nchi hii ya Gileadi, waichukue, iwe yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akawaambia, Kwamba wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu aliyevaa silaha kwa vita, mbele za BWANA, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa watu wa Gadi na wa Rubeni watavuka muto Yordani pamoja nanyi wakiwa na silaha zao chini ya uongozi wa Yawe, mukishinda na kuitwaa inchi hiyo, basi mutawapa inchi ya Gileadi ikuwe mali yao.