Numbers 33:55 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama msipowafukuza wenyeji wa nchi hiyo kwanza, basi wale mtakaowaacha watakuwa kama vibanzi machoni mwenu au miiba kila upande, na watawasumbua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wa nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama msipowafukuza wenyeji wa nchi hiyo kwanza, basi wale mtakaowaacha watakuwa kama vibanzi machoni mwenu au miiba kila upande, na watawasumbua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama miiba kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtawabakiza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mtakaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama msipowafukuza wenyeji wa nchi hiyo kwanza, basi wale mtakaowaacha watakuwa kama vibanzi machoni mwenu au miiba kila upande, na watawasumbua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini msipowafukuza mbele yenu wenyeji wa nchi hiyo, basi, hao mtakaowasaza watakuwa miiba machoni penu na machomo mbavuni penu, wawasonge ninyi katika nchi, mtakayoikaa ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama musipowafukuza wenyeji wa inchi hiyo kwanza, basi wale mutakaowaacha watakuwa kama vile sindano ndani ya macho yenu au miiba kila upande, na watawasumbua.