Numbers 34:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka Shefamu utaelekea kusini hadi Ribla, mashariki mwa Aini; kisha mpaka huo utakwenda chini hadi mteremko wa mashariki wa ziwa Kinerethi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha mpaka utatelemka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utatelemka na kufikilia upande wa bahari ya Kinerethi upande wa mashariki;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka Shefamu utaelekea kusini hadi Ribla, mashariki mwa Aini; kisha mpaka huo utakwenda chini hadi mteremko wa mashariki wa ziwa Kinerethi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye mitelemko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha mpaka utateremka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utateremka na kufikia upande wa bahari ya Kinerethi upande wa mashariki;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka Shefamu utaelekea kusini hadi Ribla, mashariki mwa Aini; kisha mpaka huo utakwenda chini hadi mteremko wa mashariki wa ziwa Kinerethi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
toka Sefamu mpaka na utelemkie Ribula na kupita Aini upande wa maawioni kwa jua; kisha mpaka uendelee kutelemka, hata ufike kando ya bahari ya Kinereti upande wake wa maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha mpaka utatelemka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utatelemka na kufikilia upande wa bahari ya Kinerethi upande wa mashariki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka Sefamu utaelekea kusini mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mupaka huo utakwenda chini mpaka kwenye muteremuko wa upande wa mashariki wa ziwa la Kinereti,