Numbers 34:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Mwenyezi Mungu ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo Bwana ameagiza wapewe watu wa zile kabila kenda, na nusu ya kabila;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. BWANA ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akawaagiza wana wa Isiraeli kwamba: Hiyo ndiyo nchi, mtakayoipata kwa kupiga kura, mwichukue, iwe yenu, naye Bwana ameagiza kuipa yale mashina tisa na nusu ya Manase.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa zile kabila kenda, na nusu ya kabila;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa akawaambia Waisraeli: Hii ndiyo inchi mutakayoirizi kwa kupiga kura, inchi ambayo Yawe ameagiza ipewe kwa makabila tisa na nusu.