Numbers 35:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miji hii itakuwa ya makimbilio kwa ajili ya Waisraeli na wageni wa kudumu au wa muda wanaokaa pamoja nao. Mtu yeyote akimuua mwingine bila kukusudia anaweza kukimbilia huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miji hii sita itakuwa mahali pa makimbilio kwa ajili ya Waisraeli, wageni na watu wengine wanaoishi kati yenu, ili mtu ambaye ameua mtu mwingine pasipo kukusudia aweze kukimbilia humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miji hiyo sita itakuwa miji ya makimbilio kwa ajili ya wana wa Israeli, na kwa ajili ya mgeni, na kwa ajili ya huyo aketiye kati yao hali ya ugeni; ili kila amwuaye mtu, naye hakukusudia kumwua, apate kukimbilia huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miji hii itakuwa ya makimbilio kwa ajili ya Waisraeli na wageni wa kudumu au wa muda wanaokaa pamoja nao. Mtu yeyote akimuua mwingine bila kukusudia anaweza kukimbilia huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miji hii sita itakuwa mahali pa makimbilio kwa ajili ya Waisraeli, wageni na watu wengine wo wote wanaoishi katikati yenu, ili kwamba mtu ye yote ambaye ameua mtu mwingine pasipo kukusudia aweze kukimbilia humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miji hii sita itakuwa mahali pa makimbilio kwa ajili ya Waisraeli, wageni na watu wengine wanaoishi katikati yenu, ili kwamba mtu yeyote ambaye ameua mtu mwingine pasipo kukusudia aweze kukimbilia humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miji hiyo sita itakuwa pa kukimbilia usalama kwa ajili ya wana wa Israeli, kwa ajili ya mgeni na kwa ajili ya aishiye nao kama mgeni; ili kila amwuaye mtu, bila kukusudia kuua, apate mahali pa kukimbilia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miji hii itakuwa ya makimbilio kwa ajili ya Waisraeli na wageni wa kudumu au wa muda wanaokaa pamoja nao. Mtu yeyote akimuua mwingine bila kukusudia anaweza kukimbilia huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miji hiyo sita iwe ya kuikimbilia wana wa Isiraeli, nao wageni, nao watakaokaa kwao, wapate kuikimbilia wote wasioua mtu kwa kusudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miji hiyo sita itakuwa miji ya makimbilio kwa ajili ya wana wa Israeli, na kwa ajili ya mgeni, na kwa ajili ya huyo aketiye kati yao hali ya ugeni; ili kila amwuaye mtu, naye hakukusudia kumwua, apate kukimbilia huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Miji hii itakuwa ya makimbilio kwa ajili ya Waisraeli na wageni wa kudumu au wa muda wanaokaa pamoja nao. Mutu yeyote akimwua mwingine bila kukusudia anaweza kukimbilia huko.