Numbers 35:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kusanyiko lazima wamlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo hadi atakapokufa kuhani mkuu aliyekuwa amepakwa mafuta matakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kutwaa kisasi cha damu; tena mkutano utamrejeza katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta kwa mafuta matakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kusanyiko ni lazima limlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo mpaka atakapokufa Kuhani Mkuu ambaye alikuwa amepakwa mafuta matakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kusanyiko ni lazima limlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo mpaka atakapokufa kuhani mkuu ambaye alikuwa amepakwa mafuta matakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kulipiza kisasi cha damu; tena mkutano utamrejesha katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta matakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumuiya itamwokoa mtu huyo aliyeua mikononi mwa jamaa ya mtu aliyeuawa, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kifo cha kuhani mkuu wa wakati huo aliyeteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wa mkutano watamponya huyo aliyeua mikononi mwake mwenye kuilipiza hiyo damu, kisha wao wa mkutano na wamrudishe katika mji wa kuukimbilia, alimokimbilia, naye atakaa humo, mpaka atakapokufa mtambikaji mkuu, waliyempaka mafuta matakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kutwaa kisasi cha damu; tena mkutano utamrejeza katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta kwa mafuta matakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baraza litamwokoa mutu huyo aliyeua toka katika mikono ya ndugu ya mutu aliyeuawa, na kumurudisha katika muji wa makimbilio alimokuwa amekimbilia. Atakaa huko mpaka kufa kwa Kuhani Mukubwa wa wakati ule aliyechaguliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.