Numbers 35:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana huyo aliyeua ni lazima akae ndani ya mji wa makimbilio mpaka kuhani mkuu atakapofariki; lakini baada ya kifo cha kuhani mkuu anaweza kurudi nyumbani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mshtakiwa lazima akae katika mji wake wa makimbilio hadi atakapokufa kuhani mkuu; atarudi tu kwenye mali yake baada ya kifo cha kuhani mkuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hata kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana huyo aliyeua ni lazima akae ndani ya mji wa makimbilio mpaka kuhani mkuu atakapofariki; lakini baada ya kifo cha kuhani mkuu anaweza kurudi nyumbani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mshtakiwa lazima akae katika mji wake wa makimbilio mpaka atakapokufa Kuhani Mkuu; atarudi tu kwenye mali yake baada ya kifo cha Kuhani Mkuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mshtakiwa lazima akae katika mji wake wa makimbilio mpaka atakapokufa kuhani mkuu; atarudi tu kwenye mali yake baada ya kifo cha kuhani mkuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hadi kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana huyo aliyeua ni lazima akae ndani ya mji wa makimbilio mpaka kuhani mkuu atakapofariki; lakini baada ya kifo cha kuhani mkuu anaweza kurudi nyumbani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ilimpasa kukaa mle mjini, alimokimbilia, mpaka mtambikaji mkuu atakapokufa. Mtambikaji mkuu atakapokwisha kufa, huyo mwuaji naye atarudi kwao kwenye fungu lake, alilolichukua, liwe lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hata kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana huyo aliyeua anapaswa kukaa ndani ya muji wa makimbilio mpaka Kuhani Mukubwa atakapokufa; lakini kisha kufa kwa Kuhani Mukubwa anaweza kurudi kwake.