Numbers 4:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eleazari mwana wa kuhani Aroni itampasa kuyatunza mafuta ya taa, ubani wa kunukia, tambiko za nafaka za kila siku, mafuta ya kupaka ili kuweka wakfu na kila kitu kilichowekwa wakfu katika hema hilo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Eleazari mwana wa Haruni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote ya Mungu na kila kitu kilicho ndani yake, pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ulinzi wake Eleazari mwana wa Haruni kuhani utakuwa ni kuyaangalia mafuta kwa nuru, na uvumba mzuri, na sadaka ya unga ya daima, na mafuta ya kupaka, tena ulinzi wa hiyo maskani yote, na wa vitu vyote vilivyo ndani yake, mahali patakatifu, na vyombo vyake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eleazari mwana wa kuhani Aroni itampasa kuyatunza mafuta ya taa, ubani wa kunukia, tambiko za nafaka za kila siku, mafuta ya kupaka ili kuweka wakfu na kila kitu kilichowekwa wakfu katika hema hilo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Eleazari mwana wa Aroni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote ya BWANA na kila kitu kilichomo ndani mwake pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Eleazari mwana wa Haruni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote ya bwana na kila kitu kilichomo ndani mwake pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ulinzi wake Eleazari mwana wa Haruni kuhani utakuwa ni kuyaangalia mafuta ya nuru, na uvumba mzuri, na sadaka ya unga ya daima, na mafuta ya kupaka, tena ulinzi wa hiyo maskani yote, na wa vitu vyote vilivyo ndani yake, mahali patakatifu, na vyombo vyake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eleazari mwana wa kuhani Aroni itampasa kuyatunza mafuta ya taa, ubani wa kunukia, tambiko za nafaka za kila siku, mafuta ya kupaka ili kuweka wakfu na kila kitu kilichowekwa wakfu katika hema hilo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kazi yake Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, ni kuyaangalia mafuta ya kinara na mavukizo yanukayo vizuri na vilaji vya tambiko vya kila siku na mafuta ya kupaka, tena kuliangalia Kao lote zima na vyote vilivyomo ndani ya Patakatifu, maana ndivyo vyombo vyake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ulinzi wake Eleazari mwana wa Haruni kuhani utakuwa ni kuyaangalia mafuta kwa nuru, na uvumba mzuri, na sadaka ya unga ya daima, na mafuta ya kupaka, tena ulinzi wa hiyo maskani yote, na wa vitu vyote vilivyo ndani yake, mahali patakatifu, na vyombo vyake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eleazari mwana wa kuhani Haruni atatunza mafuta ya taa, ubani wa kufukiza, sadaka za vyakula za kila siku, mafuta ya kupakaa kwa kutakasa na kila kitu kilichotakaswa katika hema hilo.