Numbers 4:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mapazia na kamba za ua ulio kandokando ya hema na madhabahu, mapazia ya lango la kitalu, na vifaa vyote vinavyotumika pamoja na vitu hivi. Wao watashughulika na mambo yote yanayohusika na vitu hivi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kuta za nguo za ua, na sitara ya ile nafasi ya kuingilia ya lango la ua, ulio karibu na maskani na madhabahu, kuzunguka pande zote, na kamba zake, na vyombo vyote vya utumishi wao, na yote yatakayotendeka kwavyo, watatumika katika hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mapazia na kamba za ua ulio kandokando ya hema na madhabahu, mapazia ya lango la kitalu, na vifaa vyote vinavyotumika pamoja na vitu hivi. Wao watashughulika na mambo yote yanayohusika na vitu hivi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagerishoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na pazia za nguo za ua, na sitara ya ile nafasi ya kuingilia ya lango la ua, ulio karibu na maskani na madhabahu, kuzunguka pande zote, na kamba zake, na vyombo vyote vya utumishi wao, na yote yatakayotendeka kwavyo, watatumika katika hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mapazia na kamba za ua ulio kandokando ya hema na madhabahu, mapazia ya lango la kitalu, na vifaa vyote vinavyotumika pamoja na vitu hivi. Wao watashughulika na mambo yote yanayohusika na vitu hivi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na nguo za uani na pazia la hapo pa kuingia langoni kwa ua, unaolizunguka Kao na meza ya kuteketezea ng'ombe ya tambiko, na kamba zao na vyombo vyote vya utumishi wao, nayo yote yapasayo kufanywa nao na wayafanye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kuta za nguo za ua, na sitara ya ile nafasi ya kuingilia ya lango la ua, ulio karibu na maskani na madhabahu, kuzunguka pande zote, na kamba zake, na vyombo vyote vya utumishi wao, na yote yatakayotendeka kwavyo, watatumika katika hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mapazia na kamba za upango unaokuwa kandokando ya hema na mazabahu, mapazia ya mulango wa kiwanja, na vifaa vyote vinavyotumika pamoja na vitu hivi. Wao watashugulika na mambo yote yanayoelekea vitu hivi.