Numbers 4:49 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya Mwenyezi Mungu kupitia Musa, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba. Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa amri ya Bwana, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa amri ya BWANA kupitia Mose, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba. Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama BWANA alivyomwamuru Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa amri ya bwana kupitia Musa, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba. Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama bwana alivyomwamuru Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa amri, Bwana aliyompa Mose, aliwakagua na kumweka kila mtu mmoja penye kazi yake ya utumishi na penye mzigo wake wa kuuchukua; nao wakawekwa vivyo hivyo, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mumoja alipewa kazi yake ya kufanya juu ya kubeba hema la mukutano, kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.