Numbers 5:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamweka mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfunua nywele na kumpa sadaka hiyo ya nafaka itolewayo kwa sababu ya shuku ya mumewe. Kuhani mwenyewe atashikilia kile chombo chenye maji machungu yaletayo laana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele za Mwenyezi Mungu, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za Bwana, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamweka mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfunua nywele na kumpa sadaka hiyo ya nafaka itolewayo kwa sababu ya shuku ya mumewe. Kuhani mwenyewe atashikilia kile chombo chenye maji machungu yaletayo laana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele za BWANA, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele za bwana, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za BWANA, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamweka mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfunua nywele na kumpa sadaka hiyo ya nafaka itolewayo kwa sababu ya shuku ya mumewe. Kuhani mwenyewe atashikilia kile chombo chenye maji machungu yaletayo laana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji akiisha kumsimamisha huyo mwanamke mbele ya Bwana na kuzifungua nywele za kichwani pake, na ampe mkononi mwake hicho kilaji cha tambiko cha ukumbusho, nacho ni kilaji cha tambiko cha wivu, lakini yale maji machungu yenye maapizo mtambikaji sharti ayashike mkononi mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za BWANA, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atamuweka mbele ya Yawe na kumufunua nywele na kumupa sadaka hiyo ya vyakula inayotolewa kwa sababu ya wivu wa mume wake. Kuhani mwenyewe atashikilia kile chombo chenye maji machungu yanayoleta laana.