Numbers 5:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu kuhani atamwapisha mwanamke huyo akisema: ‘Ikiwa hukulala na mwanamume mwingine, ukajitia najisi hali uko chini ya mamlaka ya mumeo, basi, hutapatwa na laana iletwayo na maji haya machungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena kwamba hukukengeuka kuandama uchafu, uli chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu kuhani atamwapisha mwanamke huyo akisema: ‘Ikiwa hukulala na mwanamume mwingine, ukajitia najisi hali uko chini ya mamlaka ya mumeo, basi, hutapatwa na laana iletwayo na maji haya machungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena ikiwa hukukengeuka kutenda maovu, ukiwa chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu kuhani atamwapisha mwanamke huyo akisema: ‘Ikiwa hukulala na mwanamume mwingine, ukajitia najisi hali uko chini ya mamlaka ya mumeo, basi, hutapatwa na laana iletwayo na maji haya machungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mtambikaji na amwapishe na kumwambia huyo mwanamke: Kama mtu hakulala kwako, nawe hukukosa na kujichafua ukimtumia mwingine kuwa kama mumeo, hutapatwa na apizo lo lote la haya maji machungu yenye maapizo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena kwamba hukukengeuka kuandama uchafu, uli chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu kuhani atamwapisha mwanamuke huyo akisema: Ikiwa haukulala na mwanaume mwingine na kujichafua wakati uko chini ya mamlaka ya mume wako, basi, hautapatwa na laana inayoletwa na maji haya machungu.