Numbers 5:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikiwa mtu huyo amefariki na hana jamaa wa karibu ambaye anaweza kupokea fidia hiyo, basi, fidia ya kosa itatolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kumfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali ya Mwenyezi Mungu, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwamba mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa Bwana kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo mume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ikiwa mtu huyo amefariki na hana jamaa wa karibu ambaye anaweza kupokea fidia hiyo, basi, fidia ya kosa itatolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kumfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali ya BWANA, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali ya bwana, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa BWANA kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo dume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikiwa mtu huyo amefariki na hana jamaa wa karibu ambaye anaweza kupokea fidia hiyo, basi, fidia ya kosa itatolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kumfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mtu huyo hakuacha ndugu anayepasa kupewa hayo malipo ya manza, sharti Bwana apewe hayo malipo ya manza, yawe yake mtambikaji, wakiisha kutoa humo dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi ya kumpatia upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwamba mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa BWANA kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo mume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ikiwa mutu huyo amekufa na hana ndugu wa karibu ambaye anaweza kupokea malipo hayo, basi, malipo ya kosa yatatolewa kwa Yawe kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kwa kumufanyia upatanisho kwa ajili ya zambi yake.