Numbers 6:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamtoa mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atamfanyia upatanisho, kwa sababu alitenda dhambi kwa ajili ya maiti. Siku hiyohiyo, atakiweka wakfu kichwa chake
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atatoa mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Mnadhiri kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwa mbele ya maiti. Siku hiyo hiyo atakiweka wakfu tena kichwa chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye kuhani atasongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa sababu aliingia kosani kwa ajili ya mfu, naye atatakasa kichwa chake siku iyo hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamtoa mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atamfanyia upatanisho, kwa sababu alitenda dhambi kwa ajili ya maiti. Siku hiyohiyo, atakiweka wakfu kichwa chake
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atatoa mmoja kama sadaka ya dhambi, na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwepo mbele ya maiti. Siku iyo hiyo atakiweka wakfu kichwa chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atatoa mmoja kama sadaka ya dhambi, na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwepo mbele ya maiti. Siku iyo hiyo atakiweka wakfu kichwa chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye kuhani atasongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa sababu aliingia kosani kwa ajili ya maiti, naye atatakasa kichwa chake siku hiyo hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamtoa mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atamfanyia upatanisho, kwa sababu alitenda dhambi kwa ajili ya maiti. Siku hiyohiyo, atakiweka wakfu kichwa chake
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji na amtumie mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ampatie upozi, kwa kuwa kosa lilimpata hapo penye yule mfu; siku hiyo sharti aseme tena, ya kama kichwa chake ni kitakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye kuhani atasongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa sababu aliingia kosani kwa ajili ya mfu, naye atatakasa kichwa chake siku iyo hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atamutoa mumoja kuwa sadaka kwa ajili ya zambi na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atamufanyia ibada ya upatanisho, kwa sababu alitenda zambi kwa sababu ya maiti. Siku hiyohiyo atatakasa kichwa chake