Numbers 6:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hiyo ndizo sheria inayomhusu mnadhiri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Mwenyezi-Mungu ilingane na nadhiri yake, licha ya chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na nadhiri aliyoweka, kadiri ya sheria ya kujiweka wakfu kwake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwa Mwenyezi Mungu kufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya chochote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea Bwana kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hiyo ndizo sheria inayomhusu mnadhiri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Mwenyezi-Mungu ilingane na nadhiri yake, licha ya chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na nadhiri aliyoweka, kadiri ya sheria ya kujiweka wakfu kwake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwa BWANA kufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya cho chote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwa bwana kufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya chochote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea BWANA kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuifuata sheria ya kujitenga kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hiyo ndizo sheria inayomhusu mnadhiri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Mwenyezi-Mungu ilingane na nadhiri yake, licha ya chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na nadhiri aliyoweka, kadiri ya sheria ya kujiweka wakfu kwake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo maongozi ya mtu atakayejieua na kuapa; haya ndiyo matoleo yake, atakayomtolea Bwana kwa ajili ya weuo wake. Kama yako mengine, mkono wake uwezayo kuyafikisha, ayatoe, basi, na ayatoe; lakini hayo, aliyoyaapa, sharti ayamalize vivyo hivyo, kama alivyoapa, na kuyafuata haya maongozi ya weuo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea BWANA kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiyo ndiyo sheria inayoelekea munaziri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Yawe ilingane na kiapo chake, zaidi ya kitu chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na kiapo alichoweka, kadiri ya sheria ya kujitakasa kwake.