Numbers 6:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu hadi kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa Bwana, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya BWANA, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya BWANA kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimguse kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zote za maapo ya weuo wake wembe usije kichwani pake; mpaka siku zitimie, alizojieua kuwa wake Bwana, sharti awe mtakatifu na kuziacha nywele za kichwani pake, zikue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku zote za kiapo chake cha kujitenga, hatanyoa nywele zake. Mpaka muda wa kiapo chake cha kujitakasa kwa Yawe utakapomalizika, atakuwa mutakatifu, ataacha nywele zake zikuwe ndefu.