Numbers 6:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hata kama ni ya baba, mama, ndugu au dada yake, asije akajitia unajisi kwa maana amejiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa kiapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hatajitia unajisi kwa ajili ya baba yake, wala kwa ajili ya mamaye, wala kwa nduguye mume, wala kwa umbu lake, wakifa wao; kwa sababu ya huku kujiweka kwa Mungu ni juu ya kichwa chake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hata kama ni ya baba, mama, ndugu au dada yake, asije akajitia unajisi kwa maana amejiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa kiapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hatajitia unajisi kwa ajili ya baba yake, wala kwa ajili ya mamaye, wala kwa kaka yake, wala kwa dada yake, wakifa wao; kwa sababu ya huku kujiweka kwa Mungu ni juu ya kichwa chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hata kama ni ya baba, mama, ndugu au dada yake, asije akajitia unajisi kwa maana amejiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa kiapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asijipatie uchafu kwa baba yake, wala kwa mama yake, wala kwa kaka yake, wala kwa mdogo wake, wala kwa umbu lake, wakifa, kwani weuo wa Mungu wake uko kichwani pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hatajitia unajisi kwa ajili ya baba yake, wala kwa ajili ya mamaye, wala kwa nduguye mume, wala kwa umbu lake, wakifa wao; kwa sababu ya huku kujiweka kwa Mungu ni juu ya kichwa chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
hata kama ni ya baba, mama, ndugu au dada yake, kusudi asijichafue kwa maana amejitakasa kwa Yawe kwa kiapo.