Numbers 6:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Endapo nywele za mnadhiri zitatiwa unajisi mtu afapo ghafla karibu naye, atakinyoa kichwa chake wakati wa siku ya kutakaswa kwake; atakinyoa katika siku ya saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kama mtu yeyote akifa ghafula karibu na Mnadhiri, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama mtu ye yote akifa ghafla karibu naye, akajitia unajisi kichwa cha kutengwa kwake, ndipo atakinyoa kichwa siku hiyo ya kutakaswa kwake, atakinyoa siku ya saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Endapo nywele za mnadhiri zitatiwa unajisi mtu afapo ghafla karibu naye, atakinyoa kichwa chake wakati wa siku ya kutakaswa kwake; atakinyoa katika siku ya saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama mtu ye yote akifa ghafula karibu naye, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama mtu yeyote akifa ghafula karibu naye, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama mtu yeyote akifa ghafla karibu naye, akajitia unajisi kichwa cha kutengwa kwake, ndipo atakinyoa kichwa siku hiyo ya kutakaswa kwake, atakinyoa siku ya saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Endapo nywele za mnadhiri zitatiwa unajisi mtu afapo ghafla karibu naye, atakinyoa kichwa chake wakati wa siku ya kutakaswa kwake; atakinyoa katika siku ya saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikiwa, inatukia, asipoviwazia, mara mtu afe hapo alipo, atakuwa amekwisha kukipatia uchafu kichwa chake kilicho na weuo wa Bwana; kwa hiyo sharti azinyoe nywele za kichwani pake siku hiyo, atakapokuwa ametakata, ndio siku ya saba, ndipo azinyoe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama mtu ye yote akifa ghafla karibu naye, akajitia unajisi kichwa cha kutengwa kwake, ndipo atakinyoa kichwa siku hiyo ya kutakaswa kwake, atakinyoa siku ya saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mutu anakufa kwa rafla karibu na munaziri na kuchafua nywele zake, huyu munaziri atanyoa kichwa chake wakati wa siku ya kutakaswa kwake; atakinyoa katika siku ya saba.