Numbers 7:17 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe waume wawili, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Nasoni, mwana wa Aminadabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe waume wawili, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.