Numbers 7:67 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kadiri ya vipimo vya hema takatifu; sahani na bakuli vilikuwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sadaka aliyoleta ilikuwa: sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sadaka yake ilikuwa: sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kadiri ya vipimo vya hema takatifu; sahani na bakuli vilikuwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kadiri ya vipimo vya hema takatifu; sahani na bakuli vilikuwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)