Numbers 7:87 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumla ya wanyama wote wa sadaka ya kuteketezwa ilikuwa mafahali kumi na wawili, kondoo madume kumi na wawili, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja kumi na wawili, pamoja na sadaka ya nafaka na beberu kumi na wawili kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo dume kumi na wawili, na wana-kondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Beberu kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ng'ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng'ombe waume kumi na wawili, na hao kondoo waume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi waume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumla ya wanyama wote wa sadaka ya kuteketezwa ilikuwa mafahali kumi na wawili, kondoo madume kumi na wawili, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja kumi na wawili, pamoja na sadaka ya nafaka na beberu kumi na wawili kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo waume kumi na wawili na wana-kondoo waume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo dume kumi na wawili na wana-kondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ng'ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng'ombe dume kumi na wawili, na hao kondoo dume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi dume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumla ya wanyama wote wa sadaka ya kuteketezwa ilikuwa mafahali kumi na wawili, kondoo madume kumi na wawili, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja kumi na wawili, pamoja na sadaka ya nafaka na beberu kumi na wawili kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jumla ya ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima ilikuwa: madume 12 ya ng'ombe, mmadume 12 ya kondoo, wana kondoo wa mwaka mmoja 12 pamoja na vilaji vyao vya tambiko; tena madume 12 ya mbuzi kuwa ng'ombe za tambiko za weuo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ng’ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng’ombe waume kumi na wawili, na hao kondoo waume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi waume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili;