Numbers 8:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
halafu Aroni atawaweka hao mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa kutoka kwa Waisraeli wanihudumie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haruni atawaweka Walawi mbele za Mwenyezi Mungu wawe sadaka ya kuinuliwa kutoka kwa Waisraeli, ili wawe tayari kuifanya kazi ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za Bwana wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe wenye kufanya utumishi wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
halafu Aroni atawaweka hao mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa kutoka kwa Waisraeli wanihudumie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aroni atawaweka Walawi mbele za BWANA kama sadaka ya kupunga kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haruni atawaweka Walawi mbele za bwana kama sadaka ya kuinua kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe watumishi wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
halafu Aroni atawaweka hao mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa kutoka kwa Waisraeli wanihudumie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Haroni na awapitishe Walawi mbele ya Bwana huku na huko, wawe kipaji cha tambiko, wana wa Isiraeli walichokitoa cha kupitishwa motoni mbele ya Bwana, wapate kuutumikia utumishi wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe wenye kufanya utumishi wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Haruni atawaweka hao mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa kutoka kwa Waisraeli wanitumikie.