Numbers 8:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walawi wakajitakasa dhambi na kuzifua nguo zao, naye Aroni akawatoa kama sadaka ya kutikiswa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Pia, Aroni alifanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walawi wakajitakasa wenyewe na wakafua nguo zao. Kisha Haruni akawasogeza mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walawi wakajitakasa na dhambi, nao wakafua nguo zao; kisha Haruni akawasongeza mbele za Bwana wawe sadaka ya kutikiswa; Haruni akafanya kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walawi wakajitakasa dhambi na kuzifua nguo zao, naye Aroni akawatoa kama sadaka ya kutikiswa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Pia, Aroni alifanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walawi wakajitakasa wenyewe na wakafua nguo zao. Kisha Aroni akawasogeza mbele za BWANA kuwa sadaka ya kupunga, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walawi wakajitakasa wenyewe na wakafua nguo zao. Kisha Haruni akawasogeza mbele za bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walawi wakajitakasa na dhambi, nao wakafua nguo zao; kisha Haruni akawasongeza mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa; Haruni akafanya kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walawi wakajitakasa dhambi na kuzifua nguo zao, naye Aroni akawatoa kama sadaka ya kutikiswa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Pia, Aroni alifanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walawi walipokwisha kujieua na kuzifua nguo zao, Haroni akawapitisha huku na huko mbele ya Bwana, kisha Haroni akawapatia upozi kwa hivyo, alivyowatakasa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walawi wakajitakasa na dhambi, nao wakafua nguo zao; kisha Haruni akawasongeza mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa; Haruni akafanya kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walawi wakajitakasa zambi na kufua nguo zao, naye Haruni akawatoa kama vile sadaka ya kutikiswa mbele ya Yawe. Vilevile, Haruni akafanya upatanisho kwa ajili yao kwa kuwatakasa.