Numbers 8:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toka sehemu za juu mpaka chini kinara hicho cha taa kilikuwa kimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kwa dhahabu iliyofuliwa kufuatana na mfano ambao Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwonesha Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambacho Mwenyezi Mungu alikuwa amemwonesha Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu tako lake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano Bwana aliokuwa amemwonyesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toka sehemu za juu mpaka chini kinara hicho cha taa kilikuwa kimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kwa dhahabu iliyofuliwa kufuatana na mfano ambao Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwonesha Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambacho BWANA alikuwa amemwonyesha Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambacho bwana alikuwa amemwonyesha Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu kitako chake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonyesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toka sehemu za juu mpaka chini kinara hicho cha taa kilikuwa kimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kwa dhahabu iliyofuliwa kufuatana na mfano ambao Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwonesha Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho kinara kilikuwa kimetengenezwa kwa kufua dhahabu; toka shina lake hata maua yake, yote pia ilikuwa kazi ya kufuafua dhahabu; kama ule mfano ulivyokuwa, Bwana aliomwonyesha Mose, ndivyo, walivyokitengeneza hicho kinara.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu tako lake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonyesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Toka sehemu za juu mpaka chini kinara hicho cha taa kilikuwa kimetengenezwa kwa ufundi mukubwa kwa zahabu iliyofuliwa kufuatana na mufano ambao Yawe alikuwa amemwonyesha Musa.