Numbers 9:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walisafiri kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya Mwenyezi Mungu Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu lilipokaa juu ya Maskani, Waisraeli walibaki kambini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa amri ya Bwana Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya Bwana walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walisafiri kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa amri ya BWANA Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa amri ya bwana Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walisafiri kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo wana wa Isiraeli waliondoka kusafiri kwa kuagizwa na Bwana, tena kwa kuagizwa na Bwana walipiga makambi. Siku zote, hilo wingu lilipokaa juu ya Kao, nao walikaa makambini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walisafiri kwa amri ya Yawe, na kupiga kambi tena kwa amri yake. Muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, watu walikaa katika kambi hiyo.