Numbers 9:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata kama wingu hilo lilikaa juu ya hema kwa muda wa siku nyingi, Waisraeli walimtii Mwenyezi-Mungu, nao hawakuondoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri ya Mwenyezi Mungu nao hawakuondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda malinzi ya Bwana, wala hawakusafiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata kama wingu hilo lilikaa juu ya hema kwa muda wa siku nyingi, Waisraeli walimtii Mwenyezi-Mungu, nao hawakuondoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri ya BWANA nao hawakuondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri ya bwana nao hawakuondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, wana wa Israeli walimtii BWANA, na hawakusafiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata kama wingu hilo lilikaa juu ya hema kwa muda wa siku nyingi, Waisraeli walimtii Mwenyezi-Mungu, nao hawakuondoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo, wingu lilipokawilia na kukaa siku nyingi juu ya Kao, wana wa Isiraeli wakamwangalia Bwana, kama ilivyowapasa kumwangalia, lakini hawakuondoka kwenda safari yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda malinzi ya BWANA, wala hawakusafiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata kama wingu hilo lilikaa juu ya hema kwa muda wa siku nyingi, Waisraeli walimutii Yawe, nao hawakuondoka.