Numbers 9:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mwingine wingu lilikaa juu ya hema tangu jioni mpaka asubuhi tu; na mara tu lilipoinuliwa, hao watu pia walifunga safari. Na ikiwa lilikaa juu ya hema mchana kutwa na usiku kucha, wao waliondoka tu wingu lilipoinuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati mwingine wingu lilikaa kuanzia jioni hadi asubuhi tu; lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Iwe ni mchana au usiku, wakati wowote wingu lilipoinuka, waliondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mwingine wingu lilikaa juu ya hema tangu jioni mpaka asubuhi tu; na mara tu lilipoinuliwa, hao watu pia walifunga safari. Na ikiwa lilikaa juu ya hema mchana kutwa na usiku kucha, wao waliondoka tu wingu lilipoinuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mwingine wingu lilikuwapo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wo wote wingu lilipoinuka, waliondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mwingine wingu lilikuwepo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wowote wingu lilipoinuka, waliondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mwingine wingu lilikaa juu ya hema tangu jioni mpaka asubuhi tu; na mara tu lilipoinuliwa, hao watu pia walifunga safari. Na ikiwa lilikaa juu ya hema mchana kutwa na usiku kucha, wao waliondoka tu wingu lilipoinuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wingu lilipokaa tu toka jioni hata asubuhi, kisha wingu lilipoondoka asubuhi, nao waliondoka kwenda safari yao; au lilipokaa tu mchana na usiku pamoja, basi, hapo wingu lilipoondoka, nao waliondoka kwenda safari yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati mwingine wingu lilikaa juu ya hema tangu magaribi mpaka asubui tu; na mara tu lilipoinuliwa, hao watu vilevile walifunga safari. Na ikiwa lilikaa juu ya hema muchana kutwa na usiku kucha, wao waliondoka tu wingu lilipoinuliwa.