Numbers 9:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walipiga kambi na kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walisafiri. Walishika agizo la Mwenyezi-Mungu kama alivyotoa amri yake kwa njia ya Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya Mwenyezi Mungu walipiga kambi, na kwa amri ya Mwenyezi Mungu waliondoka. Walitii amri ya Mwenyezi Mungu, kufuatana na agizo lake kupitia Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya Bwana walipiga kambi yao, na kwa amri ya Bwana walisafiri; wakayalinda malinzi ya Bwana, kwa mkono wa Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walipiga kambi na kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walisafiri. Walishika agizo la Mwenyezi-Mungu kama alivyotoa amri yake kwa njia ya Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa amri ya BWANA walipiga kambi, na kwa amri ya BWANA waliondoka. Walitii amri ya BWANA, kufuatana na agizo lake kupitia Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa amri ya bwana walipiga kambi, na kwa amri ya bwana waliondoka. Walitii amri ya bwana, kufuatana na agizo lake kupitia Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; walimtii BWANA, kwa mkono wa Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walipiga kambi na kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walisafiri. Walishika agizo la Mwenyezi-Mungu kama alivyotoa amri yake kwa njia ya Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo walikaa makambini kwa kuagizwa na Bwana, tena waliondoka kwenda safari yao kwa kuagizwa na Bwana. Ndivyo, walivyomwangalia Bwana, kama ilivyowapasa kuyaangalia, Bwana atakayoyaagiza kinywani mwa Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; wakayalinda malinzi ya BWANA, kwa mkono wa Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa agizo la Yawe walipiga kambi na kwa agizo la Yawe walisafiri. Walishika agizo la Yawe kama vile alivyotoa amri yake kwa njia ya Musa.