Numbers 9:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakaiadhimisha Pasaka jioni, siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli walifanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakaiadhimisha Pasaka jioni, siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli walifanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile BWANA alivyomwamuru Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile bwana alivyomwamuru Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakaiadhimisha Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakaiadhimisha Pasaka jioni, siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli walifanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakaitengeneza kondoo ya Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wakati wa jioni kule nyikani kwa Sinai; yote, Bwana aliyomwagiza Mose, wana wa Isiraeli wakayafanya vivyo hivyo sawasawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakafanya Pasaka magaribi, siku ya kumi na ine ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli wakafanya yote kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.