Obadiah 1:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku inakaribia ambapo mimi Mwenyezi-Mungu nitayahukumu mataifa yote. Kama mlivyowatendea wengine, ndivyo mtakavyotendewa, mtalipwa kulingana na matendo yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Siku ya Mwenyezi Mungu iko karibu kwa mataifa yote. Kama ulivyotenda, nawe utatendewa vivyo hivyo, matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana hiyo siku ya Bwana i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku inakaribia ambapo mimi Mwenyezi-Mungu nitayahukumu mataifa yote. Kama mlivyowatendea wengine, ndivyo mtakavyotendewa, mtalipwa kulingana na matendo yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Siku ya BWANA i karibu kwa mataifa yote. Kama ulivyofanya, nawe utafanyiwa vivyo hivyo, matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Siku ya bwana iko karibu kwa mataifa yote. Kama ulivyofanya, nawe utafanyiwa vivyo hivyo, matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku inakaribia ambapo mimi Mwenyezi-Mungu nitayahukumu mataifa yote. Kama mlivyowatendea wengine, ndivyo mtakavyotendewa, mtalipwa kulingana na matendo yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani siku ya Bwana iko karibu, iwajie wao wa mataifa yote; ndipo, utakapofanyiziwa, kama ulivyofanya, matendo yako yakikurudia kichwani pako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku inakaribia ambapo mimi Yawe nitayahukumu mataifa yote. Kama vile mulivyowatendea wengine, ndivyo mutakavyotendewa, mutalipwa kulingana na matendo yenu.