Obadiah 1:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini mlimani Siyoni watakuwapo wale waliosalimika nao utakuwa mlima mtakatifu. Wazawa wa Yakobo wataimiliki tena nchi iliyokuwa yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwa na wale watakaookoka; nao utakuwa mtakatifu, nayo nyumba ya Yakobo itamiliki urithi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini mlimani Siyoni watakuwapo wale waliosalimika nao utakuwa mlima mtakatifu. Wazawa wa Yakobo wataimiliki tena nchi iliyokuwa yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwepo na wale watakaookoka; nao utakuwa mtakatifu, nayo nyumba ya Yakobo itamiliki urithi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwepo na wale watakaookoka; nao utakuwa mtakatifu, nayo nyumba ya Yakobo itamiliki urithi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali katika mlima Sayuni kutakuwa na watakaookoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki tena milki zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini mlimani Siyoni watakuwapo wale waliosalimika nao utakuwa mlima mtakatifu. Wazawa wa Yakobo wataimiliki tena nchi iliyokuwa yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mlimani pa Sioni watakuwapo waliojiponya, napo patakuwa Patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wale waliobaki watakaa kwa mulima Sayuni nao utakuwa mulima mutakatifu. Wazao wa Yakobo watanyanganya inchi yao toka kwa wale waliokuwa wameinyanganya.