Obadiah 1:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto; nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, nao wataiwasha moto na kuiteketeza. Hakutakuwa na watakaosalimika kutoka nyumba ya Esau.” Mwenyezi Mungu amesema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yosefu itakuwa mwali wa moto; nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, nao wataiwasha moto na kuiteketeza. Hakutakuwa na watakaosalimika kutoka katika nyumba ya Esau.” BWANA amesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto; nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, nao wataiwasha moto na kuiteketeza. Hakutakuwa na watakaosalimika kutoka nyumba ya Esau.” bwana amesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa muali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walio mlango wa Yakobo watakuwa moto, nao walio mlango wa Yosefu watakuwa miali ya moto, lakini walio wa mlango wa Esau watakuwa majani makavu, ndiyo watakayoyawasha na kuyala. Kwa hiyo hawatakuwapo walio masao ya Esau, kwani Bwana ameyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa Yakobo watakuwa kama moto na wazao wa Yosefu kama ndimi za moto. Watawaangamiza wazao wa Esau kama vile moto unavyoteketeza majani yenye kukauka, hakutaponyoka hata mumoja wao. –Yawe amesema.