Philemon 1:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninakusihi kuhusu mwanangu Onesimo niliyemleta katika maisha mapya tulio nayo katika Bwana nilipokuwa gerezani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesmo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa nikiwa kifungoni mwangu, yaani, Onesimo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nakubembeleza kwa ajili ya mtoto wangu, niliyemzaa humu kifungoni mwangu; ndiye Onesimo
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakusihi kwa ajili ya mutoto wangu Onesimo, niliyemuzaa katika imani nikiwa katika kifungo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika mafungo yangu, Onesimo,