Philemon 1:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Injili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ningetamani kuendelea kuwa naye hapa, ili aendelee kunihudumia kwa niaba yako nitakapokuwa bado gerezani kwa ajili ya Habari Njema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Habari Njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Injili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye mimi nilitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako, niwapo katika kifungo kwa ajili ya Injili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Injili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nalitaka kumshika, akae kwangu, akufanyizie kazi hii ya kunitumikia humu kifungoni, nilimotiwa kwa ajili ya kuutangaza Utume mwema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ningalipenda Onesimo abakie pamoja nami kwa kunisaidia pahali pako wakati ninapokuwa mufungwa kwa sababu ya Habari Njema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambae mimi nalimtaka akae nami, apate kunikhudumia hadala yako katika mafungo ya Injili;