Philemon 1:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa hilo deni. Kumbuka kwamba nakudai hata nafsi yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mimi Paulo naandika kwa mkono wangu mwenyewe ya kwamba nitakulipa. Tena sina sababu ya kukumbusha kuwa una deni kwangu juu ya maisha yako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi Paulo, ninaandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Si kwamba ninakudai hata nafsi yako mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa. Sitaji kwamba nakudai hata nafsi yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakudai hata nafsi yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Paulo nimeviandika hivi kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitayalipa. Sitakuambia: U mdeni wangu mimi, deni lako ni moyo wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Paulo ninaandika kwa mukono wangu mwenyewe maneno haya: nitakulipa. (Sitaki kusema kwamba maisha yako ni deni unalokuwa nalo kwangu.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mimi Paoio nimeandika kwa mkouo waugu mweuyewe, nitalipa. Sikuambii kwamba wawiwa nami hatta nafsi yako.