Philemon 1:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huku nikiwa na hakika ya kutii kwako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninapokuandikia barua hii nina ujasiri mkubwa kwamba utakubaliana nami na najua kwamba utafanya zaidi ya haya ninayokuomba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale nisemayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimekuandikia, kwa sababu nimejipa moyo wa kwamba: Utatii, tena najua, ya kuwa utafanya kuyapita yale, niliyoyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninapokuandikia, nina uhakika kwamba utanisikia na hata utafanya zaidi kuliko vile nilivyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikiamini kutii kwako nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.