Philemon 1:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, upendo wako umeniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nalikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimepokea furaha kubwa na faraja kutokana na upendo wako, kwa sababu mioyo ya watu wa Mungu imepata nguvu mpya kwa juhudi zako ndugu yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, upendo wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, upendo wako umeniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nilikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, upendo wako umeniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani twalifurahi sana, mioyo yetu ikatulia kwa ajili ya upendo wako, maana roho za watakatifu umezipatia kituo wewe, ndugu yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nalikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndugu, upendo wako umenifurahisha sana na kunifariji, kwa maana umetuliza mioyo ya watu wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana tuna furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu lmeburudishwa nawe, ndugu.