Philippians 1:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haidhuru! Mimi nafurahi ikiwa tu watu wanamhubiri Kristo kwa kila njia, iwe ni kwa nia nzuri au kwa nia mbaya. Tena nitaendelea kufurahi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema, Al-Masihi anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi. Naam, nami nitaendelea kufurahi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hiyo haijalishi. Kitu cha muhimu ni kuwa wanawahubiri watu kuhusu Kristo, wakiwa na chachu safi au isiyo safi. Ninafurahi wanafanya hivyo. Nitaendelea kufurahi,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Haidhuru! Mimi nafurahi ikiwa tu watu wanamhubiri Kristo kwa kila njia, iwe ni kwa nia nzuri au kwa nia mbaya. Tena nitaendelea kufurahi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haidhuru! Mimi nafurahi ikiwa tu watu wanamhubiri Kristo kwa kila njia, iwe ni kwa nia nzuri au kwa nia mbaya. Tena nitaendelea kufurahi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema Kristo anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi. Naam, nami nitaendelea kufurahi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema, Al-Masihi anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi. Naam, nami nitaendelea kufurahi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haidhuru! Mimi nafurahi ikiwa tu watu wanamhubiri Kristo kwa kila njia, iwe ni kwa nia nzuri au kwa nia mbaya. Tena nitaendelea kufurahi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, haidhuru; inafaa, Kristo atangazwe tu kwa njia zozote, ikiwa za uwongo, au ikiwa za kweli; kwa hiyo nafurahi. Hata siku zitakazokuja nitafurahi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi si kitu! Ikiwa nia yao ni mbaya au ni nzuri habari za Kristo zinatangazwa kwa namna mbalimbali, kwa hiyo ninafurahi. Na nitaendelea kufurahi tena,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yadhuru nini? bali kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anakhubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.