Philippians 1:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Kristo Yesu, Bwana wetu, iwe pamoja nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunawatakia neema na amani toka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.