Philippians 1:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamu yangu kubwa na tumaini langu ni kwamba kwa vyovyote sitashindwa katika kutimiza wajibu wangu, bali nitakuwa na moyo thabiti kila wakati na hasa wakati huu, ili kwa maisha yangu yote, niwapo hai au nikifa, nimpatie Kristo heshima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninatarajia kwa shauku kubwa na kutumaini kwamba sitaaibika kwa njia yoyote, bali nitakuwa na ujasiri wa kutosha ili sasa kama wakati mwingine wowote, Al-Masihi atukuzwe katika mwili wangu, ikiwa ni kwa kuishi au kwa kufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama sikuzote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimejaa tumaini na uhakika, sina sababu yeyote ya kuona haya. Nina uhakika nitaendelea kuwa na ujasiri wa kuhubiri kwa uhuru kama ambavyo nimekuwa. Na Kristo atatukuzwa kwa ninayoyafanya katika mwili wangu, ikiwa nitaishi au nitakufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hamu yangu kubwa na tumaini langu ni kwamba kwa vyovyote sitashindwa katika kutimiza wajibu wangu, bali nitakuwa na moyo thabiti kila wakati na hasa wakati huu, ili kwa maisha yangu yote, niwapo hai au nikifa, nimpatie Kristo heshima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamu yangu kubwa na tumaini langu ni kwamba kwa vyovyote sitashindwa katika kutimiza wajibu wangu, bali nitakuwa na moyo thabiti kila wakati na hasa wakati huu, ili kwa maisha yangu yote, niwapo hai au nikifa, nimpatie Kristo heshima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninatarajia kwa shauku kubwa na kutumaini kwamba sitaaibika kwa njia yo yote, bali nitakuwa na ujasiri wa kutosha ili sasa kama wakati mwingine wo wote, Kristo atukuzwe katika mwili wangu, ikiwa ni kwa kuishi au kwa kufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninatarajia kwa shauku kubwa na kutumaini kwamba sitaaibika kwa njia yoyote, bali nitakuwa na ujasiri wa kutosha ili sasa kama wakati mwingine wowote, Al-Masihi atukuzwe katika mwili wangu, ikiwa ni kwa kuishi au kwa kufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama siku zote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hamu yangu kubwa na tumaini langu ni kwamba kwa vyovyote sitashindwa katika kutimiza wajibu wangu, bali nitakuwa na moyo thabiti kila wakati na hasa wakati huu, ili kwa maisha yangu yote, niwapo hai au nikifa, nimpatie Kristo heshima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hiki nacho ni kingojeo changu, nitumikiacho, kitimie: hakuna neno lo lote, ambalo nitatiwa soni nalo, ila kama vilivyokuwa kale, ndivyo, vitakavyokuwa hata sasa: Kristo atatukuzwa waziwazi po pote mwilini mwangu, ikiwa kwa njia ya kuishi au ya kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama sikuzote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kama vile ninavyongojea na kutumainia sana, sitafezeheka hata kidogo. Lakini tangia sasa na hata siku zote, nitamutukuza Kristo kwa uhodari katika maisha yangu, ikiwa nitaishi au nitakufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.