Philippians 1:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msiwaogope maadui zenu, bali muwe hodari daima, na hiyo itawathibitishia kwamba wao watashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungu mwenyewe ndiye anayewapeni ushindi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa, na hii ni kazi ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na hamtawaogopa wale walio kinyume nanyi. Imani yenu thabiti itakuwa kama ishara kwao ya kuangamia kwenu. Lakini kwa hakika ni ishara ya wokovu wenu. Na hiki ni kipawa kutoka kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msiwaogope maadui zenu, bali muwe hodari daima, na hiyo itawathibitishia kwamba wao watashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungu mwenyewe ndiye anayewapeni ushindi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msiwaogope maadui zenu, bali muwe hodari daima, na hiyo itawathibitishia kwamba wao watashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungu mwenyewe ndiye anayewapeni ushindi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa na hii ni kazi ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa, na hii ni kazi ya Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lolote; kwao hao ni ishara thabiti ya kuangamizwa, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msiwaogope maadui zenu, bali muwe hodari daima, na hiyo itawathibitishia kwamba wao watashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungu mwenyewe ndiye anayewapeni ushindi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo halitapatikana neno lo lote, wapigani wenu wanaloweza kuwatisha; napo ndipo, wanapojulika kuwa wenye upotevu, nanyi kuwa wenye wokovu, naye mwenye kuwajulisha kuwa hivyo ni Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musiogope waadui zenu hata kidogo. Hii itakuwa kitambulisho kwao kwa kuhakikisha kwamba wanapotea, lakini kwenu ni kwamba munaokolewa. Na hii inatoka kwa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu.