Philippians 2:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama kukiwa na jambo lolote la kutia moyo katika kuunganishwa na Al-Masihi, kukiwa faraja yoyote katika upendo wake, kukiwa na ushirika wowote na Roho wa Mungu, kukiwa na wema wowote na huruma,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Fikirini kuhusu kile ambacho tulichonacho kwa sababu tunamilikiwa na Kristo: hamasa aliyotuletea, faraja ya upendo wake, ushirika katika Roho wake, huruma na wema aliotuonyesha. Ikiwa mnazifurahia baraka hizi,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama kukiwa na jambo lo lote la kutia moyo, kukiwako faraja yo yote katika upendo, kukiwa na ushirika wo wote katika Roho, kukiwa na wema wo wote na huruma,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama kukiwa na jambo lolote la kutia moyo katika kuunganishwa na Al-Masihi, kukiwa faraja yoyote katika upendo wake, kukiwa na ushirika wowote na Roho, kukiwa na wema wowote na huruma,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo mlivyo naye Kristo, nawabembeleza kwamba: Ikiwa mwatulizana mioyo kwa kupendana, ikiwa m wenye roho moja, au ikiwa m wenye mioyo ya kuoneana uchungu na huruma,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maisha yenu katika kuungana kwenu na Kristo si yanawatia ninyi nguvu? Nao upendo wake si unawafariji ninyi? Si munaishi katika ushirika na Roho Mutakatifu? Si muko na moyo mwema na wa huruma?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI ikiwako faraja iliyo yote katika Kristo, yakiwako ma, tulizo yo yote ya mapenzi, ikiwako huruma yo yote na rehema,