Philippians 2:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili msiwe na lawama wala hatia, bali mwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika kizazi chenye ukaidi na kilichopotoka, ambacho ndani yake ninyi mnang’aa kama mianga ulimwenguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nanyi mtakuwa watoto wa Mungu wasiolaumiwa na wasio na hatia. Ijapokuwa mnaishi mkiwa mmezungukwa na watu wasio waaminifu wasiojali thamani haki. Katikati ya watu hao mnang'ara kama mianga katika ulimwengu wenye giza,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtang'ara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili msiwe na lawama wala hatia, bali mwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika kizazi chenye ukaidi na kilichopotoka, ambacho ndani yake ninyi mnang'aa kama mianga ulimwenguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili msiwe na lawama wala hatia, bali mwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika kizazi chenye ukaidi na kilichopotoka, ambacho ndani yake ninyi mnang’aa kama mianga ulimwenguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mtu asione la kuwaonya, mkiwa wenye hilo Neno moja tu! Hivyo mtakuwa wana wa Mungu wakaao pasipo kilema katikati yao wa ukoo huu wenye uangamizi na upotovu. Katikati yao ndiko, mnakoangaza, kama mianga inavyoangaza ulimwenguni,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kusudi mupate kuwa bila kosa na kuwa na maisha safi. Hivi mutakuwa watoto wakamilifu wa Mungu wasiokuwa na kilema kati ya watu waovu na wapotovu wa dunia hii. Munapaswa kuangaza kati ya watu hawa kama vile nyota zinavyoangaza katika mbingu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala ndanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, na kilichopotoka; kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima;