Philippians 2:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kuungana na Bwana Yesu ninalo tumaini kwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habari zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Natumaini katika Bwana Isa kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate kufarijika moyo nitakapopata habari zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa baraka za Bwana Yesu, ninategemea kuwa nitamtuma Timotheo kwenu hivi karibuni. Naye atarejesha kwangu taarifa kuhusu ninyi ili nifurahi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika kuungana na Bwana Yesu ninalo tumaini kwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habari zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kuungana na Bwana Yesu ninalo tumaini kwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habari zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate kufarijika moyo nitakapopata habari zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Natumaini katika Bwana Isa kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate kufarijika moyo nitakapopata habari zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika kuungana na Bwana Yesu ninalo tumaini kwamba nitaweza kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili nitiwe moyo kwa kupata habari zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namngojea Bwana Yesu, aitikie, nimtume Timoteo upesi kwenu, moyo wangu upate kutulia ukitambua, mambo yenu yalivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama Bwana Yesu akitaka, ninangojea kisha muda kidogo kuwatumia Timoteo, kusudi nipate kutiwa moyo na habari nitakazopata kutoka kwenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walakini natmnaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwemi karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.