Philippians 2:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi wenyewe mwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeye na mimi, kama vile mtoto na baba yake, tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana ametumika pamoja nami kwa kazi ya Injili, kama vile mwana kwa baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnafahamu Timotheo amejithibitisha kuwa ni mtu wa aina gani. Ametumika pamoja nami katika kuhubiri Habari Njema kwa njia ambavyo mwana angemtumikia baba yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nyinyi wenyewe mwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeye na mimi, kama vile mtoto na baba yake, tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi wenyewe mwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeye na mimi, kama vile mtoto na baba yake, tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana amefanya kazi ya Injili pamoja nami kama vile mwana kwa baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana ametumika pamoja nami kwa kazi ya Injili, kama vile mwana kwa baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi wenyewe mwafahamu jinsi Timotheo alivyo thabiti; yeye na mimi, kama vile mtoto na baba yake, tumefanya kazi pamoja kwa ajili ya Injili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yeye mmemtambua, ya kuwa ni mwelekevu, kwani kama mtoto anavyomtumikia baba yake, vivyo hivyo ameitumikia kazi ya kuutangaza Utume mwema pamoja nami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munajua ninyi wenyewe namna Timoteo alivyojionyesha kwamba anastahili, kwa maana alitumika kazi ya kueleza Habari Njema pamoja nami kama vile mwana anavyotumika na baba yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mwajua ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.