Philippians 2:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimeona sina budi kumtuma kwenu ndugu yetu Epafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini na vitani na ambaye ni mjumbe wenu aliyenisaidia katika mahitaji yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nadhani ni muhimu kumtuma tena kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mtendakazi pamoja nami, aliye askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma ili ashughulike na mahitaji yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa sasa, nadhani ni lazima nimrudishe Epafrodito kwenu. Ni mtumishi na mtenda kazi pamoja nami na askari mwenzangu katika jeshi la Bwana. Nilipotaka msaada, mlimtuma kwangu. Kama mjumbe wenu, alinihudumia mahitaji yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimeona sina budi kumtuma kwenu ndugu yetu Epafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini na vitani na ambaye ni mjumbe wenu aliyenisaidia katika mahitaji yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimeona sina budi kumtuma kwenu ndugu yetu Epafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini na vitani na ambaye ni mjumbe wenu aliyenisaidia katika mahitaji yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nadhani ni muhimu kumtuma tena kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mtenda kazi pamoja nami, aliye askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma ili ashughulike na mahitaji yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nadhani ni muhimu kumtuma tena kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mtendakazi pamoja nami, aliye askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma ili ashughulike na mahitaji yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini niliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mfanyakazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimeona sina budi kumtuma kwenu ndugu yetu Epafrodito, ambaye ni mwenzangu kazini na vitani na ambaye ni mjumbe wenu aliyenisaidia katika mahitaji yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nalishurutishwa moyoni kumtuma Epafurodito kwenu; yeye ni ndugu na mwenzangu wa kazi na wa vita; kisha ni mtume wenu anayenipatia yenye kunitunza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliona vema kuwatumia ndugu yetu Epafrodito, anayeshiriki pamoja nami katika kazi na katika vita ya Habari Njema. Ni yeye ndiye muliyetumia kwa kunisaidia kufuatana na mahitaji niliyokuwa nayo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini naliona imenilazimu kumtuma Epafrodito, ndugu yangu, mtendaji wa kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mkhudumu wa muhitaji yangu.