Philippians 3:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninaendelea kupiga mbio kuelekea mwisho wa mashindano ili niweze kushinda tuzo ambayo Mungu ameniitia kutoka mbinguni kwa njia ya Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nakaza mwendo, niifikie tuzo la thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nakaza mbio, nifike upesi kwenye mwisho wa kushindania, kwenye tunzo lililoko juu kwake Kristo Yesu, nililoitiwa na Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo ninakaza mwendo mpaka mwisho nipate kupokea ile zawadi Mungu aliyotuitia katika mbingu kwa njia ya Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.